Na sema: Alhamdulillah, Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye hana mwana, wala hana mshirika katika ufalme, wala hana rafiki wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa. 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na useme, «Shukrani zote ni za Mwenyezi Mungu, ukamilifu na sifa njema ni Zake, Aliyeepukana na mwana na mshirika katika uungu Wake. Na Mwenyezi Mungu Hana msaidizi yoyote kati ya viumbe vyake, Yeye Ndiye Mkwasi na Ndiye Mwenye nguvu., na wao ndio mafukara wanaomhitajia.» Na umtukuze matukuzo yaliyotimu, kwa kumsifu, kumuabudu Peke Yake bila ya mshirika, na kumtakasia Dini yote.»